Karibu

Karibu kwenye Tovuti ya CIL. Ligi ya Kutengwa inatoa huduma kwa Kaka na Dada za Christadelphian, na familia zao, ambao wametengwa na eklesia yao. Huduma hutolewa kwa ombi la eklesia yako, hata hivyo unaweza kufikia nyenzo zetu zote kwenye tovuti hii, iwe umejitenga au la.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Mawaidha ya mara kwa mara, Mafunzo ya Biblia na Mihadhara
  • Shule ya Jumapili na Shughuli za Vijana
  • Majarida ya Braille, vitabu na mawasiliano
  • Maktaba ya Rekodi za sauti na video
  • jukwaa la mikutano ya mtandaoni (CIL Meet)

Tafadhali wasiliana nasi ili kujua zaidi.

Ili kupata nyenzo zetu kwenye wavuti yetu, tafadhali jiandikishe na uingie . Unaweza kuona hakikisho hapa chini!

Makala ya hivi majuzi

Ubatizo, Nuru na Uzima

Sunday, 19 May 2024
Katika somo letu la Yoshua leo, tunakabiliana na picha moja isiyo ya kawaida. Kikundi kidogo cha makuhani Walawi, wakiwa wanalishikilia Sanduku la Agano, wamesimama ndani ya mto Yordani. Baada ya miaka 40 ya kulipita eneo la nyika (au jangwa), Israeli walikuwa tayari kuiingia Nchi ya Ahadi iliyoahidiwa kwa mababa zao zamani; nchi ijaayo maziwa na asali (Kutoka 3:17). Nasaha ya Yoshua kwao ilikuwa ni amri; anawaamuru:  “Jitakaseni, maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu” (Yosh. 3:5).

Mawimbi ya Maisha

Sunday, 12 May 2024
Msitari wa kwanza wa Matendo 27 unatuambia kuwa, akida mmoja aliyeitwa Yulio anatweka tanga kwenye meli. Yupo na wafungwa kadhaa aliokabidhiwa, akiwepo mtume Paulo. Safari inakuwa mbaya kutokana na upepo kuwa mkubwa baharini. Paulo anasema kungekuwa na hatari, lakini wanatweka tanga na kukumbana na mawimbi makubwa. Upepo mkali unaisuka-suka meli; meli inaanza kuingia maji. Pale inapokingwa na kisiwa kidogo, mabaharia wanapitisha kamba ndefu kuizunguka na kuifunga. Wanalishusha tanga kubwa, lakini sasa meli tayari inashindikana kudhibitika, kwa kuwa ilikuwa ikipigwa na dhoruba.

Kukesha

Sunday, 5 May 2024
Tukiwa watumishi wa Yesu, tunapaswa tuwe tayari tukikesha kungoja kurudi kwake. Katika wakati huo wa Nuhu watu walikuwa ‘bize’ na maisha yao ya kawaida, lakini gharika ilikuja ikawastukiza na wakaangamia. Ni waaminifu wachache tu; Nuhu na familia yake, waliookoka.

Somo kutoka katika Bustani ya Edeni

Sunday, 28 April 2024
Tukiwa tumesoma kitabu chote cha Mwanzo hivi karibuni, nilijaribu kufikiria maisha katika Bustani ya Edeni yalivyokuwa. Adamu na Hawa walikuwa wafanye nini? Walikuwa wautumieje muda wao? Mwanzo sio kitabu cha hadithi; ni kitu kilichotokea! Sisi ni sehemu ya huo ukweli, tukiwa ni uzao wa Adamu. Pale Mungu alipoziumba mbingu na nchi na vitu vyote, aliacha mpaka katika siku ya sita, ndipo alipomuumba mtu.

Uchaguzi wa Israeli, na wetu

Sunday, 21 April 2024
Katika Kumb. la Torati 28 Musa anaweka wazi sana kuwa, kulikuwa na namna mbili tu za Israeli kumwitikia Mungu; ama kumtii au kutomtii. Hapakuwa na nafasi ‘ya pembeni’. Aliwaambia kuwa uchaguzi wowote wanaoufanya, ungekuwa na matokeo yake ya moja kwa moja kwao. Utii ungeleta mibaraka na ufanisi na utajiri, wakati kutomtii kungeleta kwa vyovyote laana, kukwama na uharibifu kwao. Fursa ya kuchagua waliyopewa Israeli, iko na sisi mbele yetu. Kwetu imetolewa kwa namna tofauti kwa kuwa mazingira yanatofautiana.

Ulishaji wa watu 5,000

Sunday, 14 April 2024
Katika somo letu la Agano Jipya la Yohana 6, ndani yake upo ulishaji wa watu elfu tano. Huu ni muujiza pekee uliofanywa na Yesu, ulioandikwa kwenye Injili zote nne. Kabla hatujaangalia undani wa muujiza huo, ni muhimu kulielewa tukio la kutisha lililokuwa limetokea hivi karibuni. Ni tukio la kifo cha Yohana Mbatizaji, kitakachokuwa kilimpa huzuni sana Yesu na moyo mzito.